Sunday, 31 August 2014

Simba yaachana na Donald Musoti.

Simba yaachana na Donald Musoti.

Musoti alijiunga na Simba ,akitokea Gor Mahia ya Kenya na aliweza kuisaidia timu hiyo kwenye baadhi ya mechi za msimu uliopita japo timu hiyo ilimaliza nafasi ya nne.

KLABU ya Simba imefikia uamuzi wa kuvunja mkataba wa miaka miwili na beki wake wa kimataifa raia wa Kenya Donald Musoti na nafasi yake ameichukua Emmanuel Okwi aliyesajiliwa akitokea Yanga.
Goal inafahamu kuwa Simba imekamilisha usajili wa miezi sita kwa beki Sharifu Hassani aliyekuwa akichezea timu iliyoshuka daraja ya Ashanti United,ikiwa ni muda mchache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
“Kamati yetu ya Utendaji pamoja na benchi la ufundi kwa pamoja tumekubaliana kuachana na Musoti ili tumpe nafasi mshambuliaji mpya tuliyemsajili kutoka Yanga Emmanuel Okwi, pia tumesajili beki mpya Sharifi Hassani ambaye sasa anakwenda kuziba nafasi aliyokuwa anacheza Musoti,”alisema Makamu wa Rais wa Simba Godfrey Kaburu.
Musoti alijiunga na Simba ,akitokea Gor Mahia ya Kenya na aliweza kuisaidia timu hiyo kwenye baadhi ya mechi za msimu uliopita japo timu hiyo ilimaliza nafasi ya nne.

No comments:

Post a Comment